Kitambo nilikuwa nikipitia sms za mapenzi na kuzisoma lakini sikuona umuhimu wake. Kile kitu ambacho nilikuwa nikiaminia ni mistari yangu ambayo nitaimwaga mbele ya mwanamke. Katika maswala ya kutumia sms za mahaba hazikunigonga kichwa kabisa.
So siku moja katika pitapita zangu katika mitandao, nikakumbana na meseji moja nzuri nikaona hebu nijaribu uwezo wa meseji hii. Meseji yenyewe ilikuwa inasema hivi, "Itunze meseji hii kwa kuwa ni uthibitisho wa penzi langu kwako". Kimzaha nikamtumia mpenzi wangu aliyekuwa yuko mbali na mimi. Akajibu kupitia sms, "Asante mpenzi wangu. Nashukuru kwa mapenzi yako". Kwa kuwa sikutilia maanani na nilikuwa naamini meseji za mahaba hazina umuhimu wowote, sikushughulika.
Well, amini usiamini, baada ya mwaka mmoja na nusu niliweza kukosana na huyu mwanamke kwa sababu ya jambo dogo tu. Kilichonishangaza nikuwa ile meseji ambayo nilimtumia mwaka na unusu iliyopita kumbe bado alikuwa nayo. Mwanzo alikuwa ameisave katika sehemu maalum kwa simu yake. Nilishangazwa, nikacheka ndani yangu halafu nikamwambia, "Pole mpenzi, siwezi kuharibu penzi letu kwa sababu ya mambo madogo madogo."
Tangu hio siku nikatambua nguvu iliyopo ndani ya sms hizi za mapenzi. Zina nishati ambayo ukitumia vizuri kwa mpenzi wako, hatazisahau kwamwe. Jambo hilo lilinifanya kukusanya meseji tofauti tofauti za mapenzi na kuziweka katika kitabu kimoja ambacho kinaitwa Mahabati.
Kitabu hicho cha Mahabati tulikiandika tangu mwaka wa 2016 so ninaamini maneno hayo matamu ya mapenzi yatakuwa yametumika sana na hadi sahizi yanasaidia watu.
Tukirudi katika mada ya leo ni kuwa tumekuja na orodha ya sms za mapenzi ambazo utazitumia kwa mpenzi wako leo. Inaweza kuwa ni girlfriend wako, mke wako, rafiki yako ama yule ambaye unamfukuzia. Sms hizi zina maneno matamu ya mapenzi ambayo yanaweza kumsisimua yeyote yule ambaye utamtumia. Pia sms hizi za mahaba ndio mara ya kwanza tunazichapisha kwa mtandao hivyo nyingi zitakuwa hazijulikani na wengi. Zama nasi.
Orodha ya SMS za mapenzi
1. Kwa mpenzi wangu, wewe ni mwanamke mrembo zaidi kuliko kiumbe chochote katika maisha yangu. Nakupenda zaidi ya kitu chochote ama yeyote. Ndoto yangu ni kuwa penzi letu litaendelea kuwa na nguvu kadri siku zinavyosongea.2. Wewe ni mpenzi wangu na umenipatia sababu milioni kwa mimi kutabasamu kila siku.
3. Kwa sababu ya penzi lako, mpenzi wangu, naweza kuukwea mlima mrefu zaidi na pia kutatua matatizo makubwa zaidi. Penzi lako kwangu linayapa maisha yangu sababu za kufanikiwa.
4. Nikiwa na wewe ubavuni mwangu na penzi lako likizunguka moyo wangu, naweza kufanikiwa na chochote. Unanipa nguvu na nishati ya kukabiliana na chochote. Nakupenda kwa moyo na roho yangu.
5. Bila penzi lako katika maisha yangu, maisha yanakuwa ya upweke na kiza. Wewe ndie unayeleta mwangaza na rangi ya upinde kwa maisha yangu, hata kama ni nyakati za mawingu. Asante sana mpenzi wangu.
6. Furaha inapulizwa katika maisha yangu wakati unaponitabasamia. Unapoongea, sauti yako ina nguvu ya kunipeleka sehemu ambayo kuna upendo na amani.
7. Wewe ni mpenzi wangu bora zaidi. Wewe ni zawadi ambayo nimeletewa na Mwenyezi Mungu na nitaitunza na kuilinda daima. [Soma: Maneno 100 ya kumwambia mwanamke afurahi]
8. Mapenzi yako huyafanya maisha yangu kuwa ya mwangaza na kuvutia. Hujaacha kuamini uwezo wangu wa kutimiza mambo na kwa sababu ya hilo nakuthamini.
9. Kila dakika ninayochukua nikiwa na wewe huwa ni spesho. Tunagawa hisia zetu na maisha yetu pamoja. Hivyo napenda zile hisia zote ambazo tunakuwa nazo wakati huo. Nakupenda mpenzi wangu.
10. Nikikuweka mikononi mwangu, nahisi amani ikizunguka katika kumbata letu. Nakupenda na utakuwa karibu yangu kila wakati.
11. Kila kitu kimekamilika katika dunia yangu, hii ni kwa sababu ya penzi letu ambalo tunagawa.
12. Kila nikifunga macho yangu huwa nakuona mbele yangu. Kutengana kimwili hakuwezi kuzuia penzi letu ambalo tunalithamini tangu jadi.
13. Haijalishi mahali popote ulipo kwa kuwa mara kwa mara unakuwa ndani ya moyo wangu na fikra zangu.
14. Siku yangu huanza kwa kukufikiria wewe mpenzi wangu na huishia hivyo hivyo. Nakupenda wangu laazizi.
15. Kama ningepewa nichague kati ya kulia na wewe ama kutabasamu na mwingine, ningekuchagua wewe kila wakati. Wewe ni penzi la maisha yangu.
16. Wewe ni zaidi ya mwanamke bora kwangu, wewe ni kila kitu kwangu. Nakupenda kwa moyo wangu wote.
17. Maneno hayaji kirahisi, lakini ninapokuwa na wewe, moyo wangu unadunda kwa haraka na nyota zinangaa zaidi.
18. Laazizi wangu, wewe ni zaidi ya mchumba wangu, kila siku ni wewe unayeleta furaha ndani yangu siku baada ya siku.
19. Wewe ni chuma katika ngao yangu, upepo katika dau langu na mdundo katika moyo wangu.
20. Kwa mahabuba wangu, mpenzi wangu ninayempenda, tumekamilika tukiwa pamoja. Asante kwa kugawa maisha yako na mimi.
21. Natamani niwe kitu cha kwanza ambacho unafikiria pindi unapoamka, mpenzi wangu.
22. Itakuwa fahari yangu iwapo nitakuwa mtu wa mwisho kumfirikia kabla hujaenda kulala.
23. Una uwezo wa kumwilika maisha yangu kama vile unavyonifanyia kila siku. Nakupenda.
24. Unafanya dunia yangu kuzunguka na kuzunguka kila siku. Sijui nitafanya nini bila wewe.
[Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke katika mtandao wa Facebook]
25. Mpenzi wangu nakuhitaji kama vile moyo wangu unavyohitaji kudunda.
26. Siamini wanaposema kuwa kuna kitu kinachoitwa kupenda kwa kuona mara ya kwanza kwa sababu kila nikikuona nakupenda zaidi na zaidi.
27. Kama mimi ni mfalme katika himaya yangu, basi himaya yangu haiwezi kukamilika kama wewe hautakuwa kando yangu kama malkia.
28. Kama ningepewa nguvu za kuweza kurudisha kumbukumbu za awali, basi ningerudisha hadi ile siku ya kwanza nilipokuangalia machoni na nikakuangukia kwa kukupenda. Nakupenda mpenzi wangu.
29. Hata kama nimeshindwa kuwa chozi lako, na pia kushindwa kuwa tabasamu lako, lakini kwako umefaulu kuwa hewa yangu ambayo inanifanya kuwa hai kila siku.
30. Nataka kuwa hewa ambayo inakuzunguka kila mahali. Nataka nisitambulike lakini niwe na umuhimu zaidi kwako. Nakupenda.
31. Kuna mamilioni ya watu hapa ulimwenguni lakini wewe ndie nilikuona kuwa unanikamilisha.
32. Wewe ni kipisi ambacho nimekuwa nikikitafuta kukamilisha jedwali ambalo ni mimi.
34. Mpenzi wangu, wewe unanikamilisha kama vile ambavyo kachumbari hukamilisha pilau.
35. Wewe ni fleva katika maisha yangu. Sitaki maisha yangu yakose ladha tena, nataka ubaki na mimi mpenzi wangu.
36. Nataka kufungua macho yangu na kuangalia uso wako mrembo kila asubuhi ninapoamka. Nitakuwa mtu mwenye bahati zaidi hapa ulimwenguni.
37. Kama ningepewa uwezo wa kuondoa kitu hapa duniani, basi ningeondoa umbali kati yetu. Nakumiss sana mpenzi wangu.
38. Maisha ni mafupi so tuvunje sheria pale tunapohitaji. Napo ni tuishi kikamilivu na tupende daima.
39. Sikuwa najua kwanini haswa mtu anaweza kumuangalia mwingine na kutabasamu bila sababu zozote hadi ule wakati nilipokutana na wewe. Nataka uwe wangu.
40. Mapenzi si kitu ambacho kinaeleweka, wala pia si kitu unachokihisi, huwezi kukipokea wala kupeana, mapenzi huja tu. Ndio maana nimejikuta nimekupenda mpenzi wangu.
41. Kuna njia nyingi za kukuambia kuwa nakupenda zaidi ya chochote, lakini hakuna maneno ya kutosha kueleza jinsi ninavyokupenda.
42. Napenda kuangalia macho yako kwa kuwa yananizuzua zaidi ya kitu chochote kile ambacho nishakumbana nacho. Nataka kuwa na wewe daima dawamu.
43. Kama kukupenda wewe ni hatia, basi nihukumu.
44. Nilikuwa nakumiss hivyo nikaanza kuhisabu nyota ili niweze kutaja sababu zote ambazo zinanifanya nikumiss. Cha kushangaza nikuwa nimehisabu nyota zote nikamaliza lakini bado sababu niko nazo.
45. Nimekupatia moyo wangu kama zawadi yako, ufanyie chochote ambacho unataka kuufanyia lakini usiuvunje.
46. Nataka tuishi pamoja na kupendani kadi siku zetu za mwisho maishani.
47. Mpenzi wangu, wewe ni kama shuka katika maisha yangu, kwa hivyo usiniwache kwa hii baridi.
Tags:
MAHABA