Ok. Mmoja wa watembeleaji wa NESIMAPENZI.com kutoka Rwanda alitutumia meseji akitueleza kuwa kuna mwanamke anamfukuzia kila siku lakini ameshindwa kufunga mchezo. Amejaribu kufuata miongozo na maelekezo ya post zetu lakini hajafurahishwa na matokeo.
Baada ya kumhoji na kumuuliza maswali tulikuja kugundua kitu flani; alikuwa akilipuuza swala la mwonekano wake wa mwili.
Katika posts zetu za awali tumekuwa tukisistiza ya kuwa mwonekano wako si muhimu sana wakati wa kutongoza. Lakini je ukipatana na mwanamke ambaye kila wakati unapojaribu kumtongoza na kumshawishi anakuwa na maringo?
Jeuza na kuongeza mwonekano wako wa mwili ghafla!
Well, najua wakati ambapo unaaproach mwanamke mara ya kwanza fikra inayokuja ya kwanza ni kuwa mwanamke kama huyu asikuhukumu na vile ulivyovalia ama mwonekano wako bali aangalie tabia na maneno yako matamu ambayo utakuwa ukimwambia. Lakini kwa bahati mbaya ni kuwa wanawake wachache mno ambao wataangalia tabia yako, wengi huangalia mwonekano wako. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa ktumia sanaa ya kiza]
Leo nimeamua kuandika post hii maksudi ili tuweze kuiteka hii asilimia kubwa ya wanawake ambao huangalia mwonekano wa mtu badala ya tabia. Zama nami.
Utu wako ndicho kigezo kikuu cha kupima vile ambavyo utavalia na wala si kuangalia nguo ambazo zinatrend wa maduka au soko. Ni mara ngapi ushawaona watu unaowajua wakivalia nguo flani halafu ukasema "hizo nguo haziendani na wewe"?
Kwa wanawake wao huwa kama polisi katika fasheni, hata kama hawana taaluma hio. Ukivalia nguo ambazo haziendani na mwili wako, hazilingani na utu wako ama kutofanana na wewe utajikuta ya kuwa unatengwa ama kujiona samaki aliyetolewa baharini mbele ya wanawake. [Soma: Saikolojia kumfanya mwanamke akupende daima]
Hii ni sehemu ambayo inahitaji umakini wa hali ya juu, valia nguo ambazo zinalingana na wewe na muda si mrefu utaona wanawake wakikutambua.
2. Tafuta fasheni ambayo haipo
Fasheni ambayo si ya kawaida kama kuvalia sigha ni njia rahisi ya kupanua mwonekano wako. Unaweza kuvalia shanga, cheni, saa, pete nk ili kujenga mwonekano wako. Wasanii wengi hutumia mbinu hii ili kuvutia hadhira yao, hivyo sioni kama kuna tatizo iwapo utakuwa na mtindo huu wa mavazi. Muhimu ni umridhishe yule mwanamke ama sivyo?
3. Viatu vya maana
Usiniulize kwa nini unafaa kuachana na viatu vyako vya tangu ulipokuwa shuleni na kuanza kuvalia viatu vya fasheni. Wanawake wanakuwa na tabia ya kushangaza. Kitu cha kwaza watakacho kukuangalia ni viatu vyako. Hivyo iwapo kama unavalia viatu vya kutoboka ama vichafu hakikisha ya kuwa unafanya bajeti ya kununua viatu vipya haraka iwezekanavyo.
Unaweza kuulizia viatu vizuri vinavyokufaa katika duka ambalo utaenda kununua viatu ama unaweza kumchukua rafiki yako mwanamke akakuchagulie viatu kulingana na vile atakuona.
4. Nywele za usoni
Wakati mwingine ambapo utatembelea kinyozi hakikisha ya kuwa ndevu zako, masharubu, kionja mtuzi, nyusi (wanawake wengine huziangalia) na nywele zote kwa kichwa chako zinalingana na mwonekano, mitindo, na tabia yako. Hii ni kwa sababu zote hizi ni baadhi ya fasheni ambayo wanawake huangalia kwa umakini.
Ingawaje kunyoa kipara na ndevu zote si jambo baya, jiulize kwa nini mbona wasanii wengi wanapenda kuweka nywele za usoni na kuzishepu.
5. Safisha meno yako ama yafanye meupe
Wanawake wanatambua meno yako kwa uharaka sana hivyo unafaa kuyaweka safi na meupe. Mwanaume ambaye ni mchafu wa meno meseji anayotuma kwa mwanamke ni kuwa maisha yake ni machafu, kama utashindwa kutunza meno yako bila shaka huwezi kudumu usafi mwingine. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa ktumia sanaa ya kiza]
Pia weka kwa akili yako ya kuwa mwanamke anatarajia ya kuwa mwisho wa siku atakuwa na mwanaume ambaye anaweza kumlaza hivyo ni muhimu kuwa makini na usafi. Meno machafu, meusi ama rangi ya njano yatakufanya utengwe na wanawake mara kwa mara.
Upo!? Sasa ingia hapa uongeze makali yako.