>Nipo dukani nafikria nikununulie zawadi gani kubwa kuliko zote. >Nimeona "UPENDO" inavutia,
>pembeni nikaona tena "AMANI" inapendeza, >sijasogea nikaona "FURAHA" nikacheka nikabeba vyote, >nilipotaka kulipa mwenye duka kaniambia "MUNGU" keshanilipia, nami nimevituma kwako naomba uvipokee. Nakutakia ucku mwema!
.......................
Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje.
Hodiiiiii, Hodiiiii,
Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.