Sijui nikuekleza namna gani uelewe yaliyionijaa moyoni kwani kila nifikiriapo kwanini una walakini na hutaki kuniamini kama wewe pekee ndiye ninayekupa mahaba yangu makini, mpenzi rudisha yako imani ni wewe pekee nayekupenda hapa duniani!
Moyoni naumia kila napofikiria yale uliyonitendea, sijui nini nilikukosea kama mapenzi ya dhati naamini nilikupatia na moyoni nilikuwa najivunia na kujiona zaidi ya mfalme katika hii dunia kumbe kiini macho ulikuwa wanifanyia leo najutia muda ulionipotezea, kumbuka nilikupenda!
Nakiri kweli nimekukosea naomba msamaha kwa yote yaliyotokea hakika nimekukwaza lakini kwa kuwa hii ni yangu mara ya kwanza naamini utanisamehe la azizi na kunipa nafasi yakulienzi lako penzi.
Mpenzi nimekumiss jamani, sipati meseji wala simu sijui kwanini, nikikumbuka tunayofanyaga kitandani, natamani ungekuwa nami pembeni nakunipa mahaba yasiyo kifani, nakupenda si utani hani.
Nimezunguka pande zote za Tanzania macho nikiangaza kumsaka mrembo wakumkabidhi yangu nafsi na kulila tunda lake kwa nafasi huku nikimpa mahaba yangu ya dhati na sikuwahi kuhisi kama wewe ndiye ungeiteka yangu nafsi, nakupenda sweetie.
Tags:
MAHABA