Mimi kwako ni kipofu, nishike mkono tuvuke barabara, magari ni mengi na yanapita kwa kasi, siwezi kuona zaidi ya kusikia yakiunguruma, honi za magari siwezi kupima umbali wake, usiniache katikati ya barabara nitagongwa na kufa mara moja! Njoo niokoe nitagongwa mpenzi wangu! Forgive me dear…
Mpenzi wangu naomba unisamehe, nakupenda sana dear na ni kweli kuna wakati nakukosea, lakini amini nakupenda. Sijawahi kujuta na sitajuta kamwe kuwa na wewe! Naamini nitaendelea kuwa mwaminifu kwako, sio leo tu, bali siku zote za penzi letu!