Kila mwanaume anapenda kutaka kujua jinsi ya kumzuzua mwanamke mpaka ampende. Lakini wengi hushindwa kutimiza azma hii kwa kuwa hawajui mambo muhimu ya kufanya ili aweze kumzuzua mwanamke.
Najua labda ushawahi kuwaona mwanamke fulani wakiweza kuzuzuliwa na mwanaume, na mwanamke kama huyu anacheka mara kwa mara huku akikiri kuwa mwanaume flani anajua kuzuzua. Well, waonaje kama ni wewe sasa hivi unapewa sifa kama hii?
Kumzuzua mwanamke kutategemea uwezo wako wa kuwasiliana na yeye na kumfanya ajihisi kuwa na furaha wakati wote. Tumia mbinu tano ambazo tumezihakikisha utendaji wake.
Pokea pongezi
Wanaume wengi wanatabia ya kukataa kupokea pongezi kutoka kwa mwanamke. Balada ya wewe kuguna ama kutojiskia huru wakati mwanamke anakupongeza, mbona usitumie nafasi hii kutumia maneno ya utamu kama ile ‘asante, ‘nashukuru’ nk.
Kupokea pongezi kutoka kwa mwanamke ni kama vile kupokea zawadi kutoka kwake, hivyo kufanya hivi kutakuwa kukimfurahisha mwanamke kila wakati.
Kuwa na maoni chanya kujihusu
Kama hujiamini wewe mwenyewe ama unajiona huwezi kutimiza kumfurahisha mwanamke je unatarajia mwanamke akupende? Hivyo basi iwapo unataka kumzuzua mwanamke unafaa ujiamini wewe mwenyewe kama mwanaume
Njia rahisi ya kutimiza hii ni kuhakikisha unavalia nguo za kupendeza, unavalia marashi yakunukia, na kuwa nadhifu. Wanawake wengi wanapenda mtizamo aina hii.
Jifundishe kudensi
Ok wengi wangeuliza kwa nini nijifunze kudensi? Kudensi ina uhusiano wowote upi na kumzuzua mwanamke?
Jibu rahisi. Kwanza ni kuwa wanawake wanapenda sana wanaume ambao wanajua kudensi. Hivi ushajiuliza kwa nini dancers wengi wanapendwa na wanawake?
Pili ni kuwa wanawake wanaamini ya kuwa dancers wengi wanaujua mchezo ikija maswala ya chumbani.
Tatu ni kwa hautarajii mwanamke unayemzimia adensi na wanaume wengine wakati mumeenda kwa kilabu. So ni muhimu kujifunza kudensi, atleast style moja mbili za kumdanganya.
Isikupite Hii: Mambo 11 wasiyopenda wanaume
Tumia jina lake
Siri nyingine ya kumzuzua mwanamke ni kumtaja jina lake wakati wa maongezi. Kulingana na mwandishi maafuru wa kiingereza Dale Carnegie, anadai ya kuwa sauti tamu zaidi kwa sikio la mwanamke ni kusikia ukitaja jina lake.
Kama umekuwa ukifanya uchunguzi ni kuwa wengi wanahepa kutumia majina ya wapenzi wao nk. Hivyo wewe usikubali kuanguka ndani ya hio kategoria. Waonaje sasa uanze kutumia jina lake kila wakati unapomtext ama kuongea naye? Amini usiamini jambo hili linafanya kazi kama uchawi.
Muangazie yeye
Iwapo unataka mwanamke akuchukie kwa siku moja basi ongea na kujisifu wewe mara kwa mara wakati mnapoongea pamoja.
Iwapo unataka kumzuzua mwanamke basi kinachohitajika ni kuhakikisha unampa atenshen yako yote wakati mko pamoja mnaongea.
Kuwa mcheshi
Imethibitishwa ya kuwa hakuna mtu angependwa kujihusisha na mtu anayeboa. Hivyo kama unakipawa cha ucheshi ama unauwezo wa kumfanya mwanamke avutiwe nawe basi hio ni silaha kubwa ya kumfanya mwanamke azuzuike kwako.