Niliona si vibaya nikisoma sana biblia ili nijue ninacho paswa kukifanya kiroho kabla ya tarehe yangu ya kuzaliwa, au ndani ya hiyo siku ya natakiwa kufanyaje kiroho,namshukuru Roho mtakatifu amenisemesha mambo ya ajabu sana kwa kupitia mistari hii ya biblia.
Mhubiri 7:1 "Heri... siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa".
unaweza ukajiuliza sana kwanini maandiko yanasema heri tarehe ya kufa kuliko ya kuzaliwa,wachawi na wanajimu hawawezi kutumia tarehe ya mtu ya kufa kumlogea kwakuwa tayari amesha kufa,lakini wanaweza kutumia tarehe ya mtu ya kuzaliwa kubashiri au kumloga mtu huyo mwenye hiyo tarehe.
Nataka niwambie hakuna andiko lililo ingia kwenye biblia kwa bahati mbaya,hata kama kuna andiko unalisoma na hulielewi jua kuwa lina maana tu ya kuwepo humo.
na yenyewe biblia inatuhakikishia hilo
2Timotheo 3:14,17:
"Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki"
Kumbe basi kila jambo katika Biblia limo humo kwa sababu fulani.
Na kama kila andiko lina sababu je maandiko haya niliyo yaandika hapa chini kwa kuyanukuu kwenye biblia yanababu gani kuwepo humo kwenye biblia?
Mwanzo 40:20-22“Basi siku ya tatu ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawafanyia karamu . . . Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji kwenye cheo chake cha kunywesha . . . Lakini akamtundika (akamwua)mkuu wa waokaji.”
Andiko lingine.
Mathayo 14:6-10: “Sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode ilipokuwa ikisherehekewa binti ya Herodia alicheza dansi na kumpendeza sana Herode hivi kwamba akaahidi kwa kiapo kumpa chochote kile ambacho angeomba. Ndipo yeye, chini ya mwelekezo wa mama yake, akasema: ‘Nipe hapa juu ya sahani kichwa cha Yohana Mbatizaji.’ . . . Akatuma watu wakamkate Yohana kichwa huko gerezani.”
Kila jambo katika Biblia nimesema limo humo kwa sababu fulani.
Hapo tunaona sherehe ya kuzaliwa ya farao mtu anauwawa na kwenye sherehe ya kuzaliwa ya herode yohana mbatizaji nae anauwawa,basi nataka ujue kuna siri kubwa sana imejificha kwenye siku zetu za kuzaliwa na ndo maana wachawi na wanajimu huzitumia siku hizo kutekeleza mambo yao,na huwa nasema mara zote kitu kama hukijui haimaanishi kuwa hakipo,huwenda kikawepo na kimekugusa ila hujui.
Birthday yako ndo mwaka mpya kwako, ile January 1 ni theoretical point of time na haina uhusiano wowote na wewe.
Kila inapofika birthday yako itazame ile siku kwa mapana zaidi sababu kiuhalisia ndio siku uliyo zaliwa.
Na jua, nyota na mwezi vinakuwa kwenye position moja kama ile siku uliyo zaliwa.Ni siku ambapo dunia inakamilisha mizunguko kadhaa ya kuzunguka jua tangu uzaliwe.
Kwangu birthday siyo siku ya kufanya party bali ni siku ya kutathimini mwaka ulioisha na kupanga mipango na mikakati ya mwaka mpya ninaouanza.
Kwa wanaojifunza sana biblia wanafahamu kitu kinachoitwa lango au malango,wakati mwingine nitafundisha juu ya malango katika biblia lakini nataka utambue kuwa kuna malango,na malango hayo ni mengi,kuna lango la mzaliwa wa kwanza,lango la rehema,lango la baraka,lango la kuzimu n.k
Na kama ilivyo kwa malango hayo mengine basi SIKU YA KUZALIWA pia ni lango,linaweza kupitisha baraka au laana kwa mtu,(sisi wana wa Mungu hatujui hili nafikiri kwakuwa biblia ilituambia tumeangamia sana kwakukosa maarifa)lakini wachawi na wanajimu wanalijua hili tena kwa upana mkubwa.
Mara nyingi sisi huwaza kusherekea kukata keki na kupeana zawadi katika siku zetu za kuzaliwa,lakini kumbe kuna zaidi ya hapo...
Na wanaojua kuwa siku ya kuzaliwa inaweza kuwa lango wanajua upande mmoja tu wa mazuri,wanaamini siku ya kuzaliwa ya mtu ni lango la baraka tu,wanaamini ni siku ambayo inakuwa na furaha sana kwao na ni siku ambayo wanaweza kupokea mambo mazuri tu,lakini inawezekana wanao amini hivyo hawasomi maandiko vizuri.
Baada ya YESU tu kuzaliwa watoto wakiume waliuwawa,na baada ya MUSA tu kuzaliwa watoto wa kiume waliuwawa,kwenye sherehe ya farao ya kuzaliwa mtu alikufa,na kwenye sherehe ya kuzaliwa ya herode yohana alikufa,kama utaendelea kutazama siku ya kuzaliwa kama lango tu la kupitisha baraka utakuwa umeona kwa jicho moja.
Tarehe za kuzaliwa zimetofautiana,kwa wengine zinaweza kuwa lango la baraka na kwa wengine lango la mikosi,sasa kwakuwa watu wengi hawajui wanashangilia na kusheherekea hata siku ya mikosi.
Mhubiri 7:14"Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili....."
kuna wengine wangejua kuwa hizo siku zao ni lango la kupitia mabaya basi siku hizo nadhani keki zao wangekata huku wananena kwa lugha.
hata hivyo nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwakuwa kesho kutwa kwangu ni kama mwaka mpya,siku ya kujitathimini katika huduma na mengine...
Kama umezaliwa tarehe 26 au tarehe 8,au tarehe 17 au 4 au 22,au 13 ya mwezi wowote basi ujue kuwa hizo ni tarehe za hatari kubwa sana kwako kiroho,ni lango la mabaya,sio siku za kushangilia kwakuwa zinapitisha mikosi,uombe sana na kuchukua tahadhari kubwa sana kwakuwa utakutana na mambo mabaya katika mahusiano,uchumi na kiafya,epuka kudhurura hovyo pasipo sababu kwakuwa roho ya ajali inaweza kukufuatilia.
Wengi huzitumia hizo tarehe mwaka hadi mwaka kuzisherekea lakini huwa zinafanya kazi kama malango mwezi hadi mwezi,kama tarehe zako ni lango la baraka basi kila mwezi kwenye hiyo tarehe kuna baraka inakujia ukitambua na ukajitahidi kukaa karibu na furusa kwenye hiyo tarehe basi utashangaa sana maajabu utakayo yaona,na kama tarehe yako ni lango la mikosi basi kila mwezi hizo tarehe zitapitisha mambo machungu sana.kama tarehe yako ya kuzaliwa ina matatizo wasiliana na Mimi tufanye maombi na Mungu atakutendea muujiza katika hilo,
from SMS ZA MAHABA https://ift.tt/3CAqmjx