I miss you.

 Unayo sauti tamu, nyoka kutoka pangoni, Mejaa mashamshamu, utamu masikioni, Huniletea wazimu, kusisimuwa moyoni, U pekee duniani.

Una rangi asilia, yang'ara kama dhahabu, Rangi iliyotulia, wengine yawapa gubu,Sichoki kukusifia, wewe ndo wangu muhibu, U pekee duniani.

Macho kama ya gololi, na mapole kama njiwa, Sifa wazistahili, kwani umebarikiwa, Leo nasema ukweli, wanifanya kunogewa, U pekee duniani.









from SMS ZA MAHABA https://ift.tt/j6IOK3c

Post a Comment

Previous Post Next Post