Uwe na mchana mwema baby

 Mpenzi

Hujambo huko ulipo ? nadhani wewe ni mzima sana tena hujambo unaendelea vizuri tu , mimi sina mashaka yoyote juu yako mashaka niliyonayo ni jinsi tu unavyonimiss , najua huwa unanimiss sana , unatamani kuwa karibu na mimi muda mwingi zaidi tatizo ni huu imbali wa kimwili lakini kiroho , kihisia na kihuba tuko karibu - usijali kuhusu umbali huu kwa sababu karibuni tu tutakuwa pamoja , tutaamka katika kitanda kimoja na kulala hicho hicho , kujifunika shuka moja , kutumia sahani moja ya mlo na kushirikiana kwa kila kitu - waswahili husema tutakula vyetu .

Mpenzi

Ukimpenda mtu unatamani kufanya kila kitu ambacho kiko juu ya uwezo wako hata vile ambavyo viko juu ya uwezo wako , mimi huwa napenda kufanya vile vilivyokuwa juu ya uwezo wangu , ingawa wengine kwa ushamba na matatizo mengine huwa wanapenda kufanya yale yaliyojuu ya uwezo wao , nimeona mitaani haswa kwa baadhi ya rafiki zangu akiwa na mwanamke ndio hapo amepata njia za kujipatia malipo zaidi ya kipato chake kwa ajili ya kwenda kujichana na yule mwanamke au mpenzi wake pindi kipato kinapopungua au kuisha kabisa kwa kupunguzwa kazi au mambo kama hayo basi mapenzi pia yanaweza kupungua au kufa kabisa




Ninachotaka kusema hapa ni kwa sisi kuamua kwa nia moja kwamba mapenzi yetu yapo , yataendelea kuwepo na kudumu bila kuhusisha vipato vya mtu anavyopata au cheo cha mtu alichonacho huko kazini na sehemu zingine anazoshugulika nazo mimi nakupenda wewe kama ulivyo sio kwa ajili ya kipato chako , sio kwa ajili ya cheo chako kazini na sio kwa ajili ya umaarufu wako au familia yako au mtu yeyote anayehusiana na wewe , tuanzie hapo huko mbeleni wote tutakuwa maarufu zaidi tutakuwa na vipato zaidi , tutajenga familia bora zaidi ambazo zitakuwa mfano kwa jamii zinazotuzunguka .

Mpenzi

Mchana wa leo naomba niishie hapa , leo nina kazi nyingi kidogo nikipata nafasi nitakwandikia tena usiku wa leo kabla ya kwenda kulala , siku yangu mpaka mchana wa leo imekua salama sana pamoja na kimvua kidogo kilichonyesha hapa jijini asubuhi ya leo kimeleta Hali fulani ya hewa ambayo ni nzuri kusema za ukweli .

Kumbuka nakupenda na nitaendelea kukupenda zaidi kila siku ambazo nitaendelea kuwa hai hapa duniani hata mbinguni kama tungeruhusiwa kwenda na watu mie ningekuchagua wewe twende wote sema tu kifo kila mtu humkuta kwa wakati wake na pengi huzikwa kwa wakati wake mwenyewe .

MCHANA MWEMA , USISAHAU KWENDA KULA -- LEO NAKULA WALI NA PICHA YAKO MOYONI



from SMS ZA MAHABA https://ift.tt/AyCnWwO

Post a Comment

Previous Post Next Post