Inaweza kukuchukua miaka mitatu, minne, mitano, kumi kuja kufanikisha jambo ambalo ungetamani likamilike ndani ya mwaka mmoja.
Ndani ya miaka yote hii unakuwa ni mtu wa kujiuliza juu ya jambo moja ambalo ungetamani hata sasa likamilike au litendeke lakini inakuwa ngumu. Hapa shauku kubwa ni kutaka jambo hilo likamilike ndani ya muda unaotaka wewe.. Pamoja na shauku hiyo ulio nayo bado kuna presha inayokusuma na kuingiza hofu ndani yako..
Presha ya umri kwenda, presha ya watu wanaokutazama, presha ya watu mliokua nao, kusoma nao, presha ya watu uliowazidi umri, presha ya watu mnaoendana umri, pengine wanafanikiwa ukiwa unawaona ..lakini wewe ukijitazama bado upo chini karibu kila kitu... UPO ZERO KABISA.
Kila mmoja ana presha yake inayomsumbua ...
Mwingine presha yake ni juu ya kuwa na mume ..na akitazama umri unakwenda, alipanga kuzaa mapema tena ndani ya ndoa lakini sasa imekuwa tofauti.
Mwingine presha yake ni kuwa hana kipato cha uhakika na akijitazama hilo jambo anaona kama bado ni ndoto kwake..linamuumiza kichwa sana ..
Pengine mwingine presha yake ni vyote hana kazi maalumu, mahusihano aliyonayo hayaelewi elewi yuko njia panda ..na akitazama umri unakwenda.
Usikate tamaa ..watu wengi wametoka huko, vumilia huku ukipambana, na kama angalau kuna kipato kidogo unaingiza kuwa na despline ya pesa ...hachana na starehe zisizokusaidia kama kijana... Endelea kuangaika huku macho yako yakitazama mbele... Usiruhusu fikra zako zikakata tamaa ...maana mwanzo wa kujizika wewe mwenyewe ni pale utakapoanza kukata tamaa.
KWA BINTI AMBAE HAUJAOLEWA NA SHAUKU YAKO NI KUPATA MUME BORA
Omba sana ..narudia omba sana ...maana mume bora hapatikani ovyo kama unavyofikiri. Dunia ya sasa imejaa walaghai ...usifikiri upo salama...usalama wa maisha yako ya ndoa ya baadae imeshikiliwa na Mungu wetu.. Usiwe miongoni mwa watu wenye presha ya ndoa na kuanza kuparamia wanaume hovyo kisa unataka kuolewa kisa umri unakwenda au kisa wenzako wameolewa wote.. Umri usikuogopeshe, wenzako wameolewa wote ..kinachotakiwa kukuogopesha ni wewe kukata tamaa ya kumlilia Mungu wako ..huku ukiishi katika njia sahihi...
Usiwe na haraka ya kutaka kujibiwa maana haraka yako itakufanya ukate tamaa haraka kwa Mungu unaemuomba..
Uombapo mwambie Mungu Mapenzi yake yatimie katika maisha yako, ratiba ya maisha yako iwe ndani ya ratiba yake .. Akuongezee Amani ndani yako..maana hii ndio silaha itakayokupa matumaini kila kukicha.
Dayari Yangu
Tags:
ASUBUHI NJEMA