Wakati mwingine mwanamke ulie nae si kwamba hakupendi,si kwamba hakuhitaji,si kwamba haupo moyoni mwake,hapana bali matendo yako mambo yako machafu unayomfanyia au unayoifanyia jamii inayokuzunguka ndio tatizo linalo mtesa na kumfanya asionyeshe mapenzi kwako,asionyeshe mahaba kwako na asionyeshe tabasamu kwako.
Ubora wako usiishie tu kwako bali kuwa bora na mwema kwa mpenzi au mke wako,kuwa bora na mwema kwa familia yako na kuwa bora na mwema kwa jamii inayokuzunguka,hapo utaliona tabasamu la mwanamke huyo ulie nae,utaiona furaha ya mwanamke huyo ulie nae,utayaona mapenzi na mahaba ya mwanamke huyo ulie nae.
Kumbuka mwanamke hunena kwa vitendo 80% kama kweli unampenda kama unamhitaji fanya yale yaliyo mema kwake na kwa jamiii nzima inayokuzunguka,kumbuka thamani yako ikiwa juu ndani ya moyo wake,thamani yako ikiwa juu kwa jamii inayokuzunguka,wewe utaendelea kuwa mwanaume na mume bora siku zote.
Na mwanamke wako.atafurahia kuwa mikononi mwako daima
Tags:
MAHABA