Kutofautiana katika mahusiano si jambo jipya na geni kwa yeyote ambaye tayali yupo katika mahusiano ya kimapenzi, na inapotokea hali hii katika mahusiano, wengi hujikuta wakikosa furaha na kuumizwa na namna wanavyopata upinzani toka kwa wenzi wao kwa maneno makali na pengine kwa kutokupewa ushirikiano wowote katika jitihasda za kurejesha mahusiano mazuri kama ilivyokuwa awali.
Nimekuwa katika hali hii mara nyingi na kila nilipojaribu kumshawishi mpenzi wangu alipokuwa kanikasilikia sikupata mafanikio mazuri mapema. Na zaidi mambo yanakuwa mabaya zaidi pale ninapojaribu kutafuta muafaka. Tukiwa katika kutokuelewana na mpenzi wangu, siku moja jioni baada ya kazi za siku nilimkuta mpenzi wangu kanuna zaidi ya vile nilivyomwacha asubuhi kwa sababu za kutofautiana kwetu, nilikuwa nimechoka sana na sikutaka kutibua hasira zake zaidi kwa kujaribu kumwomba mwafaka, kwani nilijua kwa kufanya hivyo ningeharibu zaidi na kujikuna nazua yasiyozulika. Akili yangu ilitamani tu kujiburudisha na kujifariji kwa muziki na vinywaji, kasha chakula cha usiku na kulala. Na hivi ndivyo nilivyofanya, na kuna njia mbalimbali nilizoweza kuziwaza na kuzitumia kurejesha mahusiano yangu na kumfanya mpenzi wangu asiendelee kunikasililkia. Naamini njia hizi zitzweza kukufaa na wewe pia iwapo utazitumia vizuri.
Njia ya kwanza na muafaka zaidi ni kwamba usijibizane wala kujaribu kumshawishi mpenzi wako akiwa kakasilika. Jitahidi kumtuliza kwanza kwa kukubali kosa ulilolifanya na kumwomba akusamehe.
Naomba unisamhehe- ni maneno machache zaidi lakini yananguvu kubwa ya kuondoa hasira inayoweza kuleta maafa makubwa. Unaweza kuomba msamaha kwa kumaanisha au hata kwa kujifanya tu kuwa unaomba msamaha, lengo ni kwamba yaishe basi. Hautapata hasara yoyoye wala kupungukiwa chochote kwa kujishusha chini ili mambo yaishe.
Mwombe mpenzi wako mtoke nje kwa ajili ya matembezi, mpeleke maeneo rafiki huku mkizungumza mambo mbalimbali na kumbukumbu zinazoweza kuwakumbusha nyakati nzuri mlizowahi pitia mkiwa pamoja. Si mbaya iwapo mtaamua kwenda mgahawani kwa ajili ya vinywaji nyepesi, maeneo ya mapumziko, ufukweni nakadhalika. Msimulie namna siku yako ilivyokuwa ukitekeleza majukumu yako ya siku na si vibaya pia nawe ukamwuliza asimulie siku yake imekwendaje.
Haya ni mambo madogo nay a kawaida sana unayoweza kuyafanya ili kumshawishi mpenzi wako akiendelee kukukasilikia, na mimi yamenisaidia kwa kiasi kikubwa na ni imani yangu yataweza kukusaidia pia.
Zaidi kuna mbinu zingine nyepesi ambazo hutumika kutuliza hasira za wenzi wetu pale mambo yanapokuwa si mazuri,
Twanga fotooooooo, a.k.a jiselifie dudeeee, jitahidi kutumia kamera ya simu yako ya mkononi, au kamera nyingine inayoweza kufaa na kisha chukua picha pamoja na mpenzi wako. Kwa picha za mwanzo ataonekana kanuna na mwenye hasira ili tu aoneshe bado ana hasira, usihofu endelea kubadili mapozi na kutwanga maselfie yakutosha. Weka utani kidogo kisha twanga photo na jaribu kusifia picha ambazo kaonesha uchangamfu kiasi, aaaah mambo si hayoooo anapoanza kubadili hisia zake mumwagie busu mwanana katika paji lake la uso na kumwambia nilikuwa nimelimis tabasamu lako, kisha mwonyeshe tabasamu zuri, na hadi hapo tayali umemaliza kazi.
Nakutakia mafanikio mema.