Jinsi Ya Kumsisimua Mwanamke Kabla Ya Kulala Naye

 


Unapaswa kumsisimua kuanzia nafasi ya kwanza ambayo utaipata kutoka kwake. Kufanya hivyo kutamfanya akutake hata zaidi na kumfanya ajiandae na mapema kabla hata kulala naye. Lakini ni mbinu gani inayoweza kutumika kumsisimua mwanamke kabla hamjalala pamoja?


Zama nami…

Kutumia maneno
Maneno yanaweza kumsisimua mwanamke asilimia mia. Mwanzo wanawake husisimuliwa na vitu wanavyosikia zaidi kuliko wanavyoona. Hii ndio tofauti kuu kati ya jinsi ya kumsisimua mwanaume na mwanamke. Hauhitaji kuonekana mchafu wakati ambapo unamsisimua mwanamke kwa kutumia maneno. Mwanzo anaweza kusisimulika na jinsi ambavyo anakusisimua wewe. Unaweza kumwambia maneno kama “Siwezi kungojea ile siku ambayo nitakuwa pekeangu na wewe”, “Nimeanza kuingiwa na mawazo nikifikiria hio nguo uliyovaa inaficha nini” ama maneno mfanano na haya.

Lakini kando na kuwa maneno yanamsisimua mwanamke, kutategemea pia na vile ambavyo unamshika na miguso yako.

Kutumia miguso
Hapa ndipo utaleta utofauti wa yote. Miguso ni mbinu nzito na ya nguvu kama unaazimia kumfanya akutamani, kabla hata nguo za yeyote kuvuliwa, kabla ya nyinyi wawili kuanza kubusiana ama kufanya chochote. Baadhi ya mifano ya kufuata ya kumsisimua mwanamke kwa miguso ili aweze kukutamani kabla ya nyinyi wawili kulala pamoja ni kama ifuatayo: [Soma: Hatua za kumfanya mwanamke awe huru unapomgusa]

Kuzivuta nywele zake kiulaini: Usizivute nywele zake hadi ukazing’oa kichwani mwake. Lakini usiogope kuzishika baadhi ya nywele zake na kuzichezea kimvuto.

Miguso ya kukawia: Wakati ambapo unamgusa kikawaida – kwa mfano, wakati mikono yako iko katika mabega yake, mgongo au mkono – usiogope kuuzuia mkono wako ukawie sehemu hizo kwa dakika moja.

Karibu kumla dende: Hii ni siri kubwa ambayo inahakikisha gemu yako kuwa ya juu. Usikimbilie kumbusu. Jiweke katika hali ambayo nyinyi wawili mko “karibu” kubusiana. Hii itamfanya aingiwe na wazimu wa kutaka kuibusu midomo yako haraka kuliko ulivyokuwa ukitarajia.

Kumkwaruza kiulaini: Unapomgusa, usiogope kuzipitisha kucha zako kwa mgongo wake, nyuma ya shingo yake na sehemu mfanano na hizi. Hii unaweza kuitumia wakati ambapo mshajenga uhusiano wa ndani kati yenu.

Mtizamo wa macho: Kumuangalia mwanamke kwa macho pekee kunaweza kumfanya apandwe na mzuka. Mwangalie machoni, zaidi kuliko yeye. Kufanya hivyo kunaashiria ujiaminifu. Ijapokuwa mbinu hii haitumii miguso, inaweza kufanya kazi sawa na kama vile matumizi ya miguso kabla nyinyi wawili kulala pamoja.

Ok hizi ni baadhi ya mbinu za kumfanya mwanamke asisimke kabla kulala na yeye

Post a Comment

Previous Post Next Post