Je! Kama Mke akikudanganya utatunzaje ndoa yako?Jibu Hili Hapa



Hakuna siri kuoa ni kazi. Wachumba lazima wajifunze namna ya kutafuta suluhu na kubembeleza mawasiliano pale matatizo yanapotokea. Kama mwanya wa uaminifu ukitokea kwa mke wako kwaajili ya udanganyifu alioufanya mwezi wa kike, usaliti huu unaweza kupelekea kukosa 


matumaini, huzua hasira na huondoa uaminifu kabisa kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke. Watu wanaotarajia kuanza uhusiano wa kiuchumba ni vyema kutafuta washauri ili kuwashauri juu vitu vitakavyotokea vitakavyo sababisha ukosefu wa uaminifu na pia mambo yatakayo pelekea kuondoa matumaini lakini pia kuwashauri namna ya kutatua migogoro itayotokea ili kuwarudisha katika mahusiano mazuri yakayowafanya kuwa pamoja, inaweza ikasaidia.


1, Kukatisha Mawasiliano.

 Kama mke amekudanganya wewe mme, lakini hupenda kuendelea kuishi katika ndoa, kwa kawaida amekosa na amekuondolea heshima. Mbali na kumshushia heshima mumewe lakini hutakiwa kusitisha mawasiliano kwa yule ambaye walishiriki kumdanganya na kuepuka maeneo yote ambayo yatampelekea kukutana au kumkimbilia huyo mtu. Hii ni kwasababu mwanamke anatakiwa kujisikia kuwa tatizo la udanganyifu limekwisha na hata hisia zinazopelekea kukumbuka yaliyopita. .


2,Imarisha mawasiliano.

 Ingawa inaweza kuumiza na kuumiza kujadili udanganyifu au ukosefu wa uaminifu uliotendeka, ndoa inatakiwa kujengewa msingi wa ukweli na uwazi. Kuimarisha mawasiliano juu ya jambo lilitokea ambalo likapelekea udanganyifu, na inaweza kuwa ngumu sana kulijadili hili jambo kwa undani, lakini kwasababu ya kuweka amani ya moyo ni vizuri. Kama mke anaendelea kutunza siri hii italeta tatizo kubwa badala yake anatakiwa kuomba radhi na kuthamini hisia za mume wake ili kuweka ndoa yake katika hali nzuri.


3,Anzisha mahusiano upya. 

Baada ya udanganyifu, ni vigumu sana kurudisha uhusiano kama ulivyokuwa mwanzo. Katika kurudisha uamuzi wenu dhabiti, muanze uhusiano upya. Mwanamke anaweza kumshtukiza mume wake na vitu vipya vitakavyoimarisha kama kumjali, upendo ulioboreshwa yaani zaidi ya mwazo, hata kumkubatia kumbatia wakati wakiwa wote. Pale mwanamke anapomdanganya mwanaume, mwanaume hujisikia kuwa kutotakiwa katika jamii aliyopo na pia kutokuwa na mvuto. Kuwa nae karibu na kuonyesha jinsi uliyoathirika katika jambo hilo kunamuinua na kumuongezea ujasiri na kujiamini pia.

4,Tafuta washauri wa ndoa. 

Kufanya kazi na hisia za ndani za mtu aliyedanganywa na mke inahitaji mtu aliyebobea katika ushauri kuhusu maswala ya mahusiano. Mshauri wa ndoa au wa familia yeye atawasaidia wote katika kutatua migogoro na kutokuelewana kwenu, na pia hata tabia mbaya za uvunjifu wa ndoa yenu na kuwapa njia bora zitakazofanya uhusiano wenu au ndoa yenu kuuendelea, na itawasaidia kuwa na mtu wa tatu ambaye atawasikiliza na kuwapa majibu yatakayoisaidia ndoa yako.


Post a Comment

Previous Post Next Post